OR-TAMISEMI yatoa orodha ya walioitwa kazini

DODOMA-Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali za kada za afya waliowasilisha maombi katika kipindi cha mwezi wa Aprili, 2023 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilika kwa awamu ya tatu..Bofya hapa kusoma orodha ya walioitwa kazini》》》

Awamu hii ni kwa ajili ya kujaza nafasi wazi za Watumishi waliokosa ajira awamu zote 2 za awali, Ikumbukwe kuwa Ajira hizi ni za Mkataba ya miaka 2, hivyo wataalamu wote watakaojiriwa katika awamu hii wataingia mikataba na Wakurugenzi wa Halmashauri husika.

Mwezi Aprili, 2023 Ofisi ya Rais – TAMISEMI ilipata kibali cha ajira ya watumishi 8,070 wa kada mbalimbali za Afya. Nafasi ambazo zilipata waombaji wa kutosha na kupelekea kubaki kwa baadhi ya waombaji wenye sifa katika kanzi data ya OR TAMISEMI, kutokana na maombi kuzidi idadi ya kibali..Bofya hapa kusoma orodha ya walioitwa kazini》》》

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imefanikiwa kutumia kanzi data ya waombaji wenye sifa waliokuwa wamebaki katika mfumo na kuwapangia vituo vya kazi watumishi 275 katika Halmashauri mbalimbali.

Ieleweke kwamba ajira hizi ni za Mkataba kati ya Halmashauri husika na mtaalamu husika. Mkataba huu utasimamiwa na OR TAMISEMI wakati wa utekelezaji wa Mpango wa Uwekezaji katika Afya ya Mama na Mtoto yaani Tanzania Martenity and Child Health Investment program (TMCHIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia. Gharama za malipo ya mishahara zitazingatia taratibu za ajira Serikalini.Bofya hapa kusoma orodha ya walioitwa kazini》》》

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news