Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Boniphace Luhende atembelea mabanda mbalimbali Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea Dodoma

Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende, akiwasili kwenye viwanja vya Nyerere Square alipotembelea mabanda ya wadau mbalimbali wanaoshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea Jijini Dodoma kwa lengo la kuona namna wadau hao wanavyotekeleza majukumu yao ya kila siku.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende akisaini vitabu vya Taasisi zinazoshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Sheria mara baada ya kutembelea Mabanda ya Taasisi hizo kwa lengo la kuona namna taasisi hizo zinavyotekeleza majumu yao ya kila siku.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende akimsikiliza Kamishna Msaidizi divisheni ya Ukaguzi na Sayansi Jinai wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Ndg. Ziliwa Machibya alipotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa Maandhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende. akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango na Ufuatiliaji wa Mahakama ya Tanzania Ndg. Sebastian Lacha alipotembelea banda la Maboresho la Mahakama ya Tanzania wakati wa Maandhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende akimsikiliza Mkemia Mwandamizi wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bi. Leticia Waitara alipotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende akiangalia vitabu vya muongozo wa kufuata wakati wa kutengeneza Sheria ndogo na majina ya Sheria kwa lugha ya Kiswahili alipotembelea Banda ya Maonesho la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma. Kulia ni Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Theresia Sanga.
Mawakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, wakitoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi waliotembelea Banda la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende akimsikiliza Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Bi. Neema Taji alipotembelea Banda la Ofisi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende akimsikiliza Kamishna Msaidizi divisheni ya Ukaguzi na Sayansi Jinai wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),Ndg. Ziliwa Machibya alipotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa Maandhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news