Rais Dkt.Mwinyi aweka wazi mwelekeo wa Zanzibar mpya, kuna ujio wa treni, teksi za baharini na mabasi ya umeme

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar mpya itakuwa na usafiri wa umma wa mabasi ya umeme, treni pamoja na teksi za baharini.

Amesema, Serikali itatiliana saini mradi wa kituo cha usafiri wa baharini eneo la Mpiga Duri tarehe 9 Januari 2024.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Januari 6,2024 alipoweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Soko kuu la Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi B , Mkoa wa Mjini Magharibi katika shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amesema ametimiza ahadi aliyoitoa kwa wafanyabiashara wakati wa kipindi cha kampeni za uchaguzi Mwaka 2020 ikiwemo kuwajengea mazingira bora ya kufanyia biashara, kuwawezesha kwa mitaji na vitendea kazi.
Vilevile ameeleza Serikali imetimiza ahadi yake kwa kutoa mikopo inayofikia bilioni 25 kuwawezesha wajasiriamali nchini na halikadhalika wavuvi, wakulima wa mwani wamepatiwa boti bila kuwasahau waendesha bodaboda.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ametoa kipaumbele kwa wafanyabiashara wa awali wa soko la Mwanakwerekwe baada ya kukamilika Mwezi Machi kati ya wafanyabiashara 5,000 watakaoingia kwenye soko hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news