Wakfu wa Thabo Mbeki wakanusha taarifa za kifo cha Rais mstaafu Thabo Mvuyelwa Mbeki

JOHANNESBURG- Wakfu wa Thabo Mbeki  umekanusha taarifa kuwa,Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mvuyelwa Mbeki amefariki. 
Awali zilisambaa taarifa kuwa, Mbeki ambaye alizaliwa Juni 18, 1942 huko Mbewukeni, East Cape alifariki Januari 2,2024 kutokana na changamoto za kiafya.
Mbeki ni Rais wa pili kuiongoza Afrika ya Kusini kuanzia Juni 14,1999 hadi Septemba 24, 2008 alipolazimishwa kujiuzulu kutoka madarakani na Chama cha ANC.

Aliwahi pia kuwa ni Makamu wa Rais, chini uongozi wa Hayati Rais Nelson Mandela kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 1999.

Vile vile, Mbeki amewahi pia kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kati ya mwaka 2002 hadi mwaka 2003.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news