Rhobi Samwelly azidi kuwa daraja la kuinuka kiuchumi kwa wanawake mkoani Mara

NA FRESHA KINASA

WANAWAKE wajasiriamali katika Kata ya Kukirango Tarafa ya Makongoro Wilaya ya Butiama mkoani Mara wameshiriki kwa wingi katika mafunzo ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na Bending ya CRDB kwa kushirikiana na Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania ili kuwapa ujuzi na maarifa ya kuendesha biashara zao.
Ni chini ya Programu ya Benki ya CRDB inayojulikana kwa jina la EMBEJU na Erasto Widows Empowerment Programme iliyo chini ya Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania ambayo inajihusisha kuwainua wanawake kiuchumi na kuwakomboa dhidi ya ukatili wa kijinsia ambavyo wamekuwa wakikabiliana navyo katika familia na jamii pia.

Baada ya mafunzo hayo wajasiriamali hao wanatarajia kunufaika na fursa ya mikopo kutoka Benki ya CRDB kupitia EMBEJU ambapo watapata mikopo kupitia vikundi vyao pasipo kutozwa riba ili kuendeleza biashara zao ziweze kukua na kuwaletea manufaa.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Januari 4, 2024 katika Kijiji cha Kiabakari ambapo Mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania, Rhobi Samwelly na maafisa kutoka Benki ya CRDB wametoa mafunzo hayo.

Rhobi Samwelly ambaye ni Mkurugenzi wa Hope for Girls and Women in Tanzania amesema, wajasiriamali wakiwa na elimu ya biashara itasaidia kukuza mitaji yao na kukua kiuchumi.
Pia amesema, ataendelea kuwaunganisha na fursa mbalimbali za mikopo bila riba ili kuchangia maendeleo yao, familia zao na jamii kwa ujumla.

Ameongeza kuwa, kupitia Taasisi ya Erasto Widows Empowerment Programme amedhamiria kuona wanawake wajasiriamali mkoani Mara wanakuwa na kipato cha kuridhisha na kuinuka kiuchumi.

Rhobi amesema, hatua hiyo itasaidia pia kuwakomboa dhidi ya vitendo vya ukatili na amewaomba wawe wabunifu na kuwa na malengo ya kukua kibiashara.

Rhoda Pastory ni mjasiriamali na mkazi wa Kiabakari wilayani humo ambapo amesema, mafunzo hayo yatawasaisia kuendesha biashara zao kitaalamu tofauti na hapo awali huku akimpongeza Rhobi Samwelly kwa kuendelea kuwaunganisha wanawake na fursa ya mikopo pamoja na elimu ambayo ni msingi wa mafanikio yao.

Jesca Matondo amesema kuwa, kukosekana kwa elimu ya ujasiriamali imekuwa ikichangia biashara za wajasiriamali kushindwa kukua na badala yake kufa. Hivyo ameishukuru CRDB na Shirika la Hope kwa kuwapiga msasa, kwani ufanisi utaongezeka katika ufanyaji wa biashara zao.
Godfrey Dioniz ambaye ni Afisa Mahusiano Biashara kutoka Benki ya CRDB Wilaya ya Serengeti amesema, kupitia Programu ya EMBEJU mikopo kwa wajasiriamali hao itatolewa bila riba ambapo kutakuwa na ada ya asilimia sita ya mkopo, na asilimia moja kwa ajili ya malipo ya bima. Na kikundi kitakuwa dhamana kwa mkopaji.

Dioniz mesema,mikopo hiyo itatolewa kupitia vikundi kwa kumkopesha mjasiriamali mmoja mmoja akiwa ndani ya kikundi ili kuhakikisha kwamba wanainuka kiuchumi kwa kuendeleza biashara zao ambazo tayari wanazo.

Amesema, wanufaika ni wanawake wajasiriamali kuanzia miaka 18 hadi miaka 60 na mwisho wa kurejesha mkopo ni mwaka mmoja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news