Simba Queens yaichakaza Yanga Princess mabao 3-1

DAR ES SALAAM-Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya watani wa jadi Yanga Princess.

Ni katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) uliopigwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Kata ya Chamazi ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Aisha Juma awapatia bao la kwanza Simba Queens dakika ya pili baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Esther Wambui kutoka upande wa kulia.

Vile vile, Aisha aliwapatia Simba Queens bao la pili dakika ya 10 baada ya kupokea pasi kutoka Wambui kabla ya kutuliza na kupiga tiktak iliyomshinda mlinda mlango wa Princess.

Neema Paul aliipatia Princess bao la kwanza dakika ya 14 kwa kichwa kufuatia mlinda mlango wa Queens, Carolyene Rufa kutoka golini bila kuchukua tahadhari wakati wa mpira wa adhabu unapigwa na Precious.

Naye Vivian Corazone aliwapatia bao la tatu Simba Queens dakika ya 49 kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi ya Elizabeth Wambui kwa mara nyingine.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa, Fatuma Issa, Aisha Juma, Ritticia Nabbosa, Asha Djafar na Danai Bhobo na kuwaingiza Diana Mnali, Koku Kipanga, Olaiya Barakat na Esther Mayala.

Ushindi huu unaifanya Queens kufikisha alama tisa ikiwa kinara baada ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza mpaka sasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news