Simba SC yaichapa Singida Fountain Gate mabao 2-0 Mapinduzi Cup

ZANZIBAR-Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imeitandika Singida Fountain Gate mabao 2-0 katika mchezo wao wa pili wa Kombe la Mapinduzi.

Ni kupitia mtanange ambao umepigwa leo Januari 3, 2023 katika Dimba la New Amaan Complex lililopo jijini Zanzibar

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku kila timu ikijaribu kutengeneza nafasi lakini safu za ulinzi zilikuwa imara kuhakikisha nyavu zao haziguswi.

Willy Onana aliwapatia Simba SC bao la kwanza dakika ya 46 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi nje kidogo ya 18.

Aidha, Luis Miqussone aliwapatia bao la pili waajiri wake hao kwa shuti kali la mguu wa kushoto dakika ya 58 baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news