VIDEO:Rais Dkt.Mwinyi afungua Maonesho ya Biashara na Uwanja wa Maonesho

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ina mpango mzuri wa kujenga majengo ya kisasa ya Maonesho ya Biashara na kuwa kivutio kikubwa kwa wadau wa biashara, taasisi na mashirika ya kitaifa na kimataifa.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipofungua Maonesho ya 10 ya Biashara Zanzibar na kuufungua rasmi uwanja huo mpya wa Maonesho Dimani Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 10 Januari 2024 katika shamrashamraza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Maonesho hayo yameshirikisha washiriki 500 kutoka taasisi za Serikali, sekta binafsi, wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wajasiriamali.
Vilevile Rais Dkt.Mwinyi ameitaka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya viwanda kulitangaza eneo jipya hilo la maonesho na kulifanya kuwa kimataifa.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amekubali ombi la kuanzishwa kitengo maalum kuendesha na kusimamia viwanja hivyo vipya.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi ameipongeza Wizara ya Biashara na Maendeleo ya viwanda kwa kuendelea kufanya miradi mikubwa ya maendeleo na kuacha alama , pia amewataka kushughulikia maendeleo ya viwanda nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news