Vyama vya siasa vyamshukuru DC wa Ubungo

DAR ES SALAAM-Viongozi wa Vyama vya Siasa Wilaya ya Ubungo wamemshukuru na kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba kwa kutambua mchango na ushirikiano wao kwa kutoa cheti cha pongezi kwa vyama vya siasa.
Pongezi hizo zimetolewa na viongozi hao baada ya DC kuwakabidhi cheti hicho cha pongezi kutokana na ushirikiano wao mzuri waliouonyesha wakati wa kupokea na kukimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2023.

Mbali na hao pia DC ametoa vyeti hivyo kwa taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali kwa kushiriki kikamilifu katika mbio za mwenge uliokimbizwa mwaka jana.

Akikabidhi vyeti hivyo kwenye kikao cha tathmini, DC Hashim amewashukuru wadau wote kwa ushirikiano mzuri walioutoa wakati wa kupokea na kukimbiza Mwenge huo wa Uhuru mwaka 2023.

"Kwa niaba ya viongozi wa serikali wilayani hapa, tunawashukuru wadau wote zikiwemo taasisi za serikali, zisizo za kiserikali, wadau wa maendeleo pamoja na viongozi wa vyama vya siasa kwa ushirikiano mliouonyesha, tunaomba muendelee na ushirikiano huo,"amesema Komba.

Komba amesema kuwa, ushirikiano na kujitoa kwa hali na mali kwa wadau mbalimbali imepelekea Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kushika nafasi ya pili kimkoa, nafasi ya 8 kikanda na kuwa ya 26 Kitaifa.

Kwa upande wake marabaada ya kupokea cheti hicho Mratibu wa Umoja wa Vyama rafiki wilayani humo kutoka Chama cha ADA TADEA, Leonard Adam amesema kuwa, kitendo cha Mkuu wa Wilaya hiyo kutoa vyeti Kwa vyama vya Siasa ni heshima kubwa sana kwao kama viongozi wa vyama na imeonyesha ni jinsi gani DC ametambua mchango wa Vyama vya Siasa.

"Tunampongeza sana DC Komba, kwani ametambua mchango wetu kama Vyama vya Siasa kwa kuwa hapo awali haijawahi kutokea viongozi wa Vyama wilayani hapa tukapewa cheti Cha pongezi Ili hali Kila mwaka tulikuwa tunashiriki," amesema.

Leonard, ameongeza kuwa cheti hicho kimewaongezea hali ya ushirikiano viongozi wa vyama hivyo na kwamba watashirikiana na serikali pale inapobidi katika kuhakikisha azma ya Ubungo waitakayo inafikiwa kwa kuwa maendeleo hayana chama.

"Tupo pamoja na tutaendelea kushirikiana na viongozi mbalimbali katika wilaya yetu pale tunapoona inafaa kufanya hivyo lengo likiwa ni kuhakikisha maendeleo ya wana Ubungo yanafikiwa."

Vyama vilivyopata cheti ni pamoja na CCK, NRA, UMD, ADA TADEA, DEMOKRASIA MAKINI, NCCR Mageuzi, UPDP, SAU, AAFP ,NLD, TLP, ADC, ACT Wazalendo, CUF, DP.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news