Waziri Makamba ateta na Waziri wa Uhamiaji nchini Bahamas

KAMPALA-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe January Makamba amekutana na Waziri wa Uhamiaji na Bima ya Taifa wa Bahamas, Mhe. Alfred M. Sears pembezoni mwa l Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) unaoendeles jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 15 hadi 20 Januari 2024.
Katika kikao hicho, Viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa nchi zao kuchukua hatua za haraka kuanzisha ushirikiano rasmi kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili.
Maeneo ya ushirikiano yatakayopewa kipaumbele ni pamoja na kukuza sekta ya utalii, biashara na Uwekezaji, michezo na utamaduni .

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news