Wananchi jitokezeni uchaguzi Serikali za mitaa-Mbunge Dkt.Cherehani

NA MATHIAS CANAL

WANANCHI wametakiwa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2024.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, MMh.Dkt.Emmanuel Cherehani ameyasema hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mbika Kata ya Ushetu na Kijiji cha Ilomelo Kata ya Ulowa.
Mbunge Cherehani pia amewahamasisha vijana na akina mama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo ili kuleta mabadiliko katika jamii.

"Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan toka ameingia madarakani tumeona mambo makubwa ya kimaendeleo aliyoyafanya.
"Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani akina mama walivyo na uwezo mkubwa katika uongozi.

"Nichukue nafasi hii kuwahamasisha mama zangu, dada zangu pamoja na vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa pindi mchakato utakapotangazwa rasmi," amesema Mbunge Cherehani.
Mhe. Cherehani pia amewataka wananchi kuchagua viongozi wenye hofu ya Mungu na wanaotaka kuwatumikia kweli kwa kuwaletea maendeleo huku akiahidi kuendelea kushirikiana na viongozi waliopo kuhakikisha wanaendelea kuboresha maisha ya wananchi katika jimbo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news