Wasiojulikana wavunja duka na kumuua mlinzi

MWANZA-Watu ambao hawakufahamika kwa haraka majina yao, wamevamia na kuvunja duka katika Mtaa wa Mwananchi, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza na kuiba vitu mbalimbali kisha kumuua mlinzi aliyekuwa lindoni.
Mlinzi huyo ameuawa kwa kushambuliwa kwa kutumia kitu chenye ncha kali katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mmoja wa wamiliki wa duka hilo, Isack William, alisema alipofika dukani huko majira ya asubuhi, walikuta makufuli yamekatwa na taa zimenyofolewa na alipofungua mlango na kuingia ndani, alibaini bidhaa zimechukuliwa na mlinzi akiwa amelala huku kichwa chake kikivuja damu.

William alisema kuwa, baada ya kushuhudia hilo, alimwita jirani yake ili amwangalie kama wanaweza kumpeleka hospitalini, lakini baada ya jirani huyo kufika walibaini alikuwa amefariki dunia, ndipo wakatoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.

Mwenyekiti wa Mtaa huo, Kata ya Buzuruga, Catherine Thomas, alitaja hatua zinazoendelea kuchukuliwa za kuhamasisha na kusimamia suala la ulinzi na usalama katika mtaa huo ili kudhibiti uhalifu wa namna hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news