Zanzibar, China kushirikiana Uchumi wa Buluu

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Januari 28,2024 amekutana na Naibu Waziri wa Maliasili wa China, Mhe.Sun Shuxian na ujumbe wake Ikulu jijini Zanzibar.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameishukuru Serikali ya China kwa misaada ambayo wamekuwa wakiipatia Zanzibar katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kudumisha uhusiano wa muda mrefu.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema, China na Zanzibar zitatiliana saini hati ya ushirikiano katika sekta ya uchumi wa buluu ikiwemo sayansi na teknolojia ya baharini.

Pia, uchunguzi wa mazingira ya bahari, utabiri wa ufuatiliaji na tahtmini ya maafa, utafiti wa baharini, kujengea uwezo, uwekezaji, uhifadhi wa viumbe hai wa baharini na ulinzi wa mfumo wa ikolojia wa baharini.

Naye Naibu Waziri wa Maliasili wa China,Mhe.Sun Shuxian ameeleza kuwa, China inatoa fursa za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Kizanzibari katika fani ya bahari na viumbe wa baharini, pia itaendeleza ushirikiano na Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news