Balozi Kasike akutana na uongozi wa Chuo Kikuu cha Eduardo Mondlane

MAPUTO- Mheshimiwa Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, amekutana na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Eduardo Mondlane cha Msumbiji ulioongozwa na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Doutor Manuel Guilherme Junior.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 13,2024 na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo, Msumbiji.
Katika mazungumzo yao, pande mbili zilikubaliana kuimarisha uhusiano na ushirikiano (kati ya Tanzania na Msumbiji) katika sekta ya Elimu, hususan kuanzishwa Darasa la Kiswahili Chuoni hapo na Darasa la Kireno katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news