Dkt.Ibrahim Msabaha afariki

DAR ES SALAAM- Aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Ibrahim Msabaha (72) amefariki.
Amefariki leo Februari 13,2024 akiwa njiani akipelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.

Dkt.Msabaha alikuwa akipelekwa hospitali baada ya hali yake ya kiafya kubadilika ghafla usiku.

Dada yake, Pili Msabaha amethibitisha hilo, Dkt.Msabaha alikuwa ni mtu wa kuumwa na kulazwa na kisha kuruhusiwa hadi mauti yalipomfika leo.

Vile vile Dkt.Msabaha amewahi kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Kibaha mkoani Pwani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news