DAR ES SALAAM-Kocha wa Simba, Abdelhak Benchikha, ameuambia uongozi wa klabu hiyo kuwa beki wake wa kati, Henock Inonga yupo kwenye mipango yake msimu huu katika mashindao ya Kimataifa na Ligi Kuu.
Inonga ambaye kwa sasa yupo na kikosi cha timu yake ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenye fainali za AFCON zinazoendelea nchini Ivory Coast, anatajwa kutakiwa na vilabu vya soka vya FAR Rabat na Berkane za Morocco.