Maafisa wa polisi waliopandishwa vyeo wapongezwa

ZANZIBAR-Kamishna wa Polisi Zanzibar,Hamad Khamis Hamad amewataka maafisa wa polisi waliopandishwa vyeo kuimarisha utawala wa sheria, katika himaya zao na kufuatilia malalamiko na changamoto za wananchi li kuzitafutia ufumbuzi.
Akiwapongeza maafisa 14 waliopandishwa vyeo na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa upande wa Kamisheni ya Polisi Zaznibar ngazi ya Naibu Kamishna wa Polisi na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi huko Kilimani Makao Makuu ya Polisi Zanzibar amewasisitiza kuweka mikakati ya kudhibiti uhalifu kwa kukuza ushirikishwaji wa jamii na kuongeza matumizi ya takwimu katika kubaini na kuzuia uhalifu.

Kwa upande wake Mkuu wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali watu Zanzibar, Naibu Kamishna wa Polisi Mhandisi Simon Thomas Chillery amesema, kupandishwa vyeo kwa maafisa hao kuende sambamba na kuimarika kwa kazi za Polisi.

Akizungumza kwa niaba ya maafisa waliopandishwa vyeo Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Naibu Kamishna wa Polisi Zuberi Chembera wamemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuliboresha Jeshi la Polisi na kuahidi kua watatumia vyeo hivyo kufanya kazi kwa kufuata sheria, kanuni na kuzingatia nidhamu , haki, weledi na uwadilifu katika majukumu yao.

Hivi karibuni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan aliwapandisha vyeo maafisa wa polisi 155 ikiwa 14 kutoka Kamisheni ya Polisi Zanzibar kati ya hao wawili ni Naibu Kamishna wa Polisi na 12 ni Kamishna Wasaidizi waandamizi wa Polisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news