Mbunge Ole Lekaita akabidhi magari ya wagonjwa Sunya

NA MATHIAS CANAL

KITUO cha Afya cha Sunya kilichopo katika Wilaya ya Kiteto kimekabidhiwa magari mawili ya wagonjwa (Ambulance) kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi magari hayo Februari 16,2024 Mbunge wa Jimbo la Kiteto mkoani Manyara, Mhe.Edward Ole Lekaita amesema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa magari hayo ili kupunguza adha wanazozipata wananchi.
Amesema,Rais Dkt.Samia ametoa magari matatu ambapo mawili kati ya hayo yamewasili mjini Kiteto, magari mawili yatakuwa kwa ajili ya wagonjwa na moja kwa ajili ya madaktari.

Mbunge Ole Lekaita amewataka wahudumu wa afya pamoja na wananchi wote kuhakikisha wanayatunza magari hayo ili yaweze kutumika kuwahudumia kama Serikali ilivyokusudia.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mhe. Iddy Kassim pamoja na Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini,Mhe.Priscus Tarimo ambao kwa pamoja wamempongeza Mbunge huyo kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kuwatumikia wananchi kwa ufasaha.
Wamewasihi wananchi kuendelea kumuunga mkono na kumuombea mbunge wao ili aendelee kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news