Mtu hapendezi kwa maombi, anapendeza akiwa na hela-Nabii Mkuu Dkt.GeoDavie

NA GODFREY NNKO

NABII Mkuu, Mheshimiwa Dkt.Geordavie wa Ngurumo ya Upako amewataka Wakristo na Watanzania kwa ujumla kutambua kuwa, mtu huwa anapendeza akiwa na fedha, hivyo kufanya kazi kwa bidii ni lazima.
Nabii Mkuu Mheshimiwa Dkt.GeoDavie wa Ngurumo ya Upako jijini Arusha.

Ameyabainisha hayo hivi karibuni katika moja wapo ya ibada iliyofanyika ndani ya Ngurumo ya Upako (Chuo Kikuu cha Manabii) iliyopo Kisongo jijini Arusha.

"Yaani unalala, unaamka unamuomba Mungu usiku, mchana, jioni. Unamuomba Mungu akupe viatu, akupe nguo, akupe chakula, akupe mahitaji yote bila kufanya kazi?.

"Wewe ni kukesha na kuomba tu, kukesha na kuomba tu...ananiongoza roho...eee...hela itaingia mfukoni kwa namna hiyo, haiwezi kuingia mfukoni, haiwezi kuingia mfukoni hela.

"Fanya kitu kwa kiasi, omba kwa kiasi, chapa kazi. Tumia muda mwingi kufanya kazi, jamani mtu hapendezi kwa maombi anapendeza akiwa na hela.

"Neno la mtumishi wako kanisani likusaidie wewe kukufanyia wepesi katika kazi za mikono yako ili uweze kupenya kwa haraka, na kufanikiwa kwa haraka.

"Huo ndiyo tunauita muujiza, lakini kutegemea neno la Nabii unasema, Nabii ameshatamka imeshakuwa, mimi ninaenda kulala ninajua Mungu atarekebisha mambo. Unamtuma Mungu akakufanyie kazi? Mungu anabariki kazi ya mikono yako.

"Yaani wewe umuombe Mungu akupe hela, yeye Mungu ndiye anaenda kufanya kazi akupe hela?. Unampa Mungu kazi, akafanye kazi akuletee wewe hela? Ee…Yaani wewe umekaa nyumbani unataka Mungu akafanye kazi akuletee hela, anafanyaje kazi?.

“Unatakiwa kufanya kazi wewe mwenyewe kwa mikono yako, na Mungu anabariki kazi ya mikono yako siyo kazi ya maombi yako.

“Mungu habariki kazi ya maombi yako, anabariki kazi ya mikono yako, yaani miujiza Mungu akupe wewe, wewe umekaa tu bwetee…kila kitu miujiza, aha… kuna vitu vingine ni kwa kufanya kazi,"alifafanua Nabii Mkuu,Mheshimiwa Dkt.Geordavie.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news