Musoma Vijijini wawekeza katika Sayansi shuleni

NA FRESHA KINASA

KATIKA kuadhimisha miaka 47 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) Wanachama wa chama hicho na wananchi kwa ujumla wa Kata ya Kiriba Wilaya ya Musoma Wameshiriki sherehe hizo na Kisha kutembelea Bwai Sekondari na kushuhudia ukamilishaji wa ujenzi wa maabara zake tatu za nasomo ya sayansi.
Ni maabara za Physics, Chemistry na Biology ambapo wamepongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita na Mbunge wao,Prof. Muhongo kwa jinsi wanavyoendelea kuimarisha sekta ya elimu jimboni humo kwa ushirikiano.

Sherehe hizo zimefanyika Kijiji cha Bwai Kumsoma Kata ya Kiriba Februari 4, 2024, ambapo wananchi pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kwa pamoja kufanya maadhimisho hayo ambayo yamefana kwa kiwango kikubwa na kisha kutembelea ujenzi wa shule hiyo.

Sekondari hii ni ya pili ya Kata ya Kiriba ambayo ujenzi wake umetokana na michango ya wananchi wa Kijiji cha Bwai Kumsoma, Mbunge wa jimbo, Prof. Sospeter Muhongo na Serikali Kuu ambayo imechangia ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwa kutoa shilingi milioni 153.

Neto Mwakyusa ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo ambapo amemshukuru Prof. Muhongo kwa hamasa kubwa kwa wananchi ambayo amekuwa akiitoa juu ya ushiriki wao ujenzi wa maabara hizo pamoja na michango yake ya fedha na vifaa vya ujenzi katika kuona kwamba masomo ya sayansi yanasomwa na wanafunzi kwa vitendo.

Rhobi Samwelly ni Mjumbe wa UWT Taifa Mkoa wa Mara ambapo amepongeza juhudi za Serikali katika kutoa fedha za ujenzi wa maabara na miradi mingine ikiwemo maji jimboni humo.

Pia ushiriki wa Prof. Muhongo, Chama Cha Mapinduzi na wananchi jimboni humo katika ajenda ya maendeleo kwa umoja.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Februari 4, 2024 imeeleza kuwa,"Sherehe za kufungua rasmi shule hii iliyoanza kutoa elimu ya sekondari mwaka jana itafanyika mwezi ujao." imeeleza taarifa hiyo.

Aidha,taarifa hiyo imeongeza kuwa uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu Musoma Vijijini. Ambapo "Wanavijiji na Mbunge wao wa Jimbo wanashirikiana na Serikali yetu kwenye ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwenye sekondari zote za Jimbo la Musoma Vijijini."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news