Mwanahabari Kazimbaya Makwega Adeladius akamatwa kwa tuhuma za kuandika taarifa za UDOM

MWANZA-Mwanahabari Kazimbaya Makwega Adeladius (Mwanakwetu) amekamatwa akiwa kazini katika Chuo cha Michezo cha Malya jijini Mwanza.
Hayo ni kwa mujibu wa mtoa taarifa kutoka chuoni hapo ambapo inadaiwa, Makwega aliandika taarifa za upotoshaji kuhusu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

"Polisi kutoka Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma walifika maeneo haya Chuo cha Michezo saa 4 asubuhi leo Februari 22,2024 kwa kufika Ofisi ya Mkuu wa Chuo cha Malya kumuhitaji mtumishi, na ndugu yetu Kazimbaya Makwega.

"Na wakaeleza dhumuni la ujio wao, na hivyo wakapata ushirikianoo wa kila kitu kutoka ofisi na kwa Makwega mwenyewe.

"Hivyo kama ndugu na jamaa wa Kazimbaya Makwega maarufu kama Mwanakwetu tambua hivyo, ila jua kwa sasa hapatikani,"amefafanua mtoa taarifa huyo kutoka Chuo cha Malya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news