Kamati yataka ushirikishwaji wa wananchi maeneo ya miradi ya elimu

NA ASILA TWAHA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewashauri watendaji wa Halmashauri kuwashirikisha wananchi kuchagua maeneo ya kupeleka miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ili kuleta tija kwa watumiaji.
Akizungumza Februari 21, 2024 kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa miradi ya elimu ya shule za awali, msingi na sekondari mkoani Morogoro, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Denis Londo, amesema kamati hairidhishwi na baadhi ya maamuzi ya watu wachache ya kuhamisha miradi bila ya kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika ambao ndio walengwa na watumiaji wa miradi hiyo.

Akitolea mfano kwa Halmashauri ya Wilaya Mvomero kubadilisha eneo la awali lililokuwa ijengwe shule ya sekondari kata ya Homboza na ujenzi wake kuhamishwa na baadhi ya watu imejengwa kata ya Manza na bila ya kuwashirikisha wananchi.

“Jambo hili sio busara sababu miradi hii inawalenga wananchi watu wachache wanaofanya maamuzi bila kuwashirikisha wananchi sio jambo zuri, watendaji wa Halmashauri acheni tabia ya kujichukulia maamuzi ambayo yanaleta migogoro kwa wananchi na nitoe wito kwa watendaji hawa kuwa wazalendo na kuweka maslahi ya wanachi na sio kwa baadhi ya watu wachache.

"Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa kwa watanzania ni jukumu letu kufanya kazi kwa maslahi ya wanachi wetu," amesema Mhe. Londo.

Kamati hiyo bado inaendelea na ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Morogoro kukagua utekelezaji wa miradi ya elimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news