Oryx yapeleka tabasamu kwa viongozi wa dini Kilimanjaro

KILIMANJARO-Viongozi wa dini nchini wameombwa kushiriki kikamilifu katika kuimasisha jamii kuchana na uharibu wa mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia ili kuondokana na uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya kuni na mkaa katika kuandaa chakula.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga( wa tatu kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo (wa kwanza kushoto),Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond (wa pili kushoto) Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro ( wa pili kulia) na Meneja Masoko wa Oryx Shaban Fundi (wa kwanza kulia) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya Oryx Ofisa Daawa wa Kata ya Msaranga iliyopo Moshi Mjini Shekhe Twahir Hussein wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 26,2024 katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro.

Ombi hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi ya Oryx 1000 pamoja na majiko yake kwa viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali mkoani Kilimanjaro yaliyokwenda sambamba na utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya matumizi ya nishati safi ili kuepuka madhara kwa jamii.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mitungi hiyo kwa viongozi wa dini na wajasiriamali Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema viongozi wa dini wanamchango mkubwa katika kusaidia jamii kutambua umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuachana kutumia kuni na mkaa.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas Shaban Fundi akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Benoit Araman wakati wa hafla ya kukawa mitungi ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini na wajasiriamali wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Shaban Fundi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Benoite Araman ametumia nafasi hiyo kueleza kwa muda mrefu sasa wamekuwa wanajivunia kuwezesha makundi mbalimbali yakiwemo wanawake, watoto na wajasiriamali kupata nishati safi ya kupikia.

Amesema kwa kufanya hivyo wanaamini wanaikomboa jamii na taifa kwa ujumla wake kwani kupika kwa gesi ya Oryx kuna maanisha kuboresha afya za kinamama kwa kueuka kuvuta moshi mbaya wa kuni na mkaa.Pia tunaweza watoto kupata muda wa kwenda shule badala ya kutumwa kutafuta kuni,”amesema Fundi.

Aidha amekumbusha kuwa mwaka 2021 Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alianzisha kampeni ya nishati safi ya kupikia na alitoa maono yake ya kwamba ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya wananchi itumie nishati safi, hivyo kuanzia hapo Oryx iliongeza nguvu na hadi sasa ya mitungi 19000 bure yenye thamani isiyopungua Sh.bilioni 1.5.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga (wa tatu kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo( wa kwanza kushoto) Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond( wa pili kushoto) Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro (wa pili kulia) na Meneja Masoko wa Oryx Shaban Fundi( wa kwanza kulia) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya Oryx Sister Piala Olomi kutoka Shirika la Masisita wa Bibi Yetu mkoa wa Kilimanjaro wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa dini ambao wamepatiwa mitungi ya gesi sambamba na kupatiwa mafunzo ya matumizi salama ya nishati hiyo, wamemshukuru mbunge Shally pamoja na Oryx kwa kutambua kundi hilo na nafasi yake katika kuhamasisha jamii kutunza mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news