Dkt.Biteko mgeni rasmi mkutano wa wadau wa utamaduni na sanaa

NA SHAMIMU NYAKI

NAIBU-Naibu Waziri Mkuu na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa Utamaduni na Sanaa utakaofanyika tarehe 29 Februari, 2024 Johari Rotana jijini Dar es Salaam  ukishirikisha wadau takribani 800 wa Tanzania Bara.
Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari leo Februari 27,2024 jijini Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa ameeleza kuwa mkutano huo ni katika kuendelea kuimarisha sekta za Utamaduni na Sanaa nchini lengo ikiwa ni kujadili kwa pamoja mwenendo wa sekta hizo pamoja na kuziboresha.
"Kupitia mkutano huo wadau wa Utamaduni na Sanaa watapata wasaa wa kujengewa uwezo,kubadilishana uzoefu, kufahamiana, kuendesha mijadala yenye afya kwa ajili ya kubainisha changamoto zinazoikabili sekta na kuweka mikakati ya kuitatua pamoja na kuwatambua na kuwatunuku wadau waliofanya vizuri katika zekta hizo," ameongeza Katibu Mkuu Msigwa.

Amesema kuwa, walengwa wa mkutano huo ni taasisi zinazojishughulisha na Utamaduni na Sanaa, taasisi za fedha, Kampuni za Bima, Washirika wa Maendeleo, Kampuni za Simu, Vyuo vya Elimu ya Kati na juu, Asasi za kiraia na Taasisi za umma na binafsi zinazojihusisha na urasimishaji wa kazi za Sanaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news