Rais Dkt.Samia afanya uteuzi TARI,HESLB na PSSSF

DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Thomas Nestory Bwana kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).
Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Bwana alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais na anachukua nafasi ya Dkt. Geofrey Mkamilo ambaye amemaliza muda wake.

Vile vile, amemteua pia aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ambapo Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba atapangiwa kazi nyingine.

Rais Dkt. Samia amemteua pia Dkt. Bill Kiwia kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) akichukua nafasi ya Badru ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news