Rais Katalin Novak ajiuzulu

BUDAPEST-Rais wa Hungary, Katalin Novak amelazimika kujiuzulu baada ya shinikizo la kumsamehe mtu aliyepatikana na hatia ya kusaidia kuficha unyanyasaji wa kijinsia katika nyumba ya watoto.
Aliyekuwa Rais wa Hungary, Katalin Novak. [File: Michal Cizek/AFP].

Katalin Novak, mshirika wa karibu wa Waziri Mkuu wa kihafidhina Viktor Orban, alijiuzulu wiki moja baada ya msamaha wake kama Rais wa Hungary kuripotiwa kwa mara ya kwanza na tovuti ya habari ya 444.

Ufichuzi huo kutoka tovuti ya 444, ulisababisha ghasia za umma na madai kutoka kwa upinzani kumtaka Katalin Novak na aliyekuwa Waziri wa Sheria wa Serikali ya Hungary, Judit Varga kujiuzulu.

Judit Varga ambaye amekuwa mwanasiasa nyota anayechipukia kutoka katika chama tawala cha Viktor Mihály Orbán cha Fidesz – Hungarian Civic Alliance, alijiuzulu kama mbunge siku ya Jumamosi.

Judit Varga alitarajiwa kuongoza orodha ya Fidesz katika uchaguzi, na ambaye pia alitia saini msamaha alieleza kupitia mtandao wa × kuwa angejiuzulu kama mbunge wa Fidesz, akiwajibika kwa uamuzi wake.

Wiki hii, vyama vya upinzani vya Hungary vilimtaka Katalin Novak ajiuzulu kutokana na kesi hiyo na Ijumaa waandamanaji elfu moja walikusanyika katika ofisi ya Novak wakimtaka ajiuzulu.

Katalin Novak alilazimika kukatisha ziara yake ya kazi Qatar, akarejea Budapest, Hungary ili awajibike kwa kujiuzulu. Matangazo ya moja kwa moja ya televisheni ya Taifa ya Hungary yakaruka hewani.

“Nilifanya makosa...leo ni siku ya mwisho kuhutubia kama Rais, nilifanya uamuzi wa kutoa msamaha Aprili 2023 nikiamini mfungwa huyo hakutumia vibaya mazingira magumu ya watoto aliowasimamia,"alinukuliwa Rais huyo. (NA)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news