TAKUKURU Songwe yawauma sikio watumishi

SONGWE-Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Songwe imetoa wito kwa watumishi wenye dhamana ya kusimamia miradi ya maendeleo kuhakikisha wanasimamia kwa ufanisi.
Wito huo umetolewa Januari 31, 2024 na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Songwe, Mohamed Shariff wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Taasisi hiyo.

Shariff amesema kuwa, ili miradi ya Serikali iweze kukamili kwa wakati na kufikia viwango vya ubora unaohitajika na kuendana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali wenye dhamani ya kusimamia wahakikishe wana simamia kikamilifu.

"Tupo hapa leo kuuhabarisha umma kuhusiana na utendaji kazi wa ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Songwe kwa kipindi cha Oktoba mpaka Disemba 2023," amesema Shariff.

Ameongeza kuwa, katika kipindi hicho uelimishaji dhidi ya rushwa umefanyika kupitia semina 43, uimarishaji wa klabu 52 za wapinga rushwa, vipindi vitano vya radio, na mikutano 56 ya hadhara.

Vilevile katika kutekeleza programu ya TAKUKURU Rafiki ambapo kero zaidi ya 230 ziliibuliwa na kati ya kero hizo 191 ziliweza kutatuliwa na zilizobaki zinaendelea kushughulikiwa

Ameongeza kuwa, TAKUKURU Mkoa wa Songwe ilishiriki maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za binadamu ambapo taasisi hiyo ilishiriki maadhimisho hayo kwa kupanda miti 1200 katika shule ya msingi Isangu wilayani Mbozi

Aidha, Naibu Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Songwe amesema, taasisi hiyo imejipanga kuendelea kutoa elimu dhidi ya rushwa, kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo kwenye uchambuzi wa mifumo na rasilimali za umma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news