Balozi Kasike ateta na Balozi wa Kenya jijini Maputo

MAPUTO- Machi 6, 2024 Mheshimiwa Phaustine M. Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Maputo alikutana na Balozi wa Jamhuri ya Kenya nchini Msumbiji, Mhe. Philip Githiora kwenye Ofisi za Ubalozi zilizopo jijini Maputo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 12, 2024 na Ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo.
Katika mazungumzo yao, Viongozi hao wawili walizungumza masuala ya Ushirikiano baina ya nchi hizi mbili katika sekta mbalimbali. Aidha, walizungumzia masuala yanayohusu Ushirikiano kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kusisitiza haja ya kuimarishwa kwa Jumuiya hiyo kwa maslahi ya nchi wanachama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news