Balozi Kasike ateta na Waziri wa Kilimo Ufalme wa Eswatini,mifugo yahitajika

MBABANE-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji,Mheshimiwa Phaustine Kasike amekutana na Waziri wa Kilimo wa Ufalme wa Eswatini, Mhe. Mandla Tshawuka.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 28,2024 na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo,Msumbiji.
Viongozi hao wamefanya mkutano katika Ofisi za Wizara ya Kilimo ya Ufalme wa Eswatini jijini Mbabane.

Kwa pamoja wamesisitiza haja ya kusainiwa Hati ya Makubaliano (MoU) itakayorasimisha mahusiano hayo na pia kueleza maeneo na namna ambavyo nchi hizi zitashirikiana katika Sekta ya Kilimo.
Kwa upande mwingine, Serikali ya Eswatini iliwasilisha ombi la kununua mifugo kutoka Tanzania, ambapo Mhe. Balozi Kasike aliahidi kulifikisha kwenye mamlaka husika kwa hatua za maamuzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news