Balozi Kasike ateta na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Msumbiji

MAPUTO-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji,Mheshimiwa Phaustine Kasike amekutana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri Msumbiji, Mhe Pascoal Pedro Joao Ronda katika ofisi za wizara hiyo zilizipo jijini Maputo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 25,2024 na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo,Msumbiji.

Katika mkutano huo, viongozi hao wawili walizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji na kujadiliana kwa undani namna ya kuimarisha ushirikiano huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news