Balozi Kasike, Waziri Dkt.Cordoso waangazia fursa Uchumi wa Buluu

MAPUTO-Mheshimiwa Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji amekutana na Mhe. Dkt. Lidia Cordoso, Waziri wa Bahari, Mito na Uvuvi wa Jamhuri ya Msumbiji kwenye ofisi za eizara hiyo jijini Maputo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 25,2024 na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijjni Maputo, Msumbiji.

Kupitia mkutano huo, viongozi hao walizungumza masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji katika Eneo la Uchumi wa Buluu hususani uvuvi na kilimo cha mazao ya Bahari.
Ili kuwezesha ushirikiano wenye tija na maslahi kwa pande zote mbili, viongozi hao walikubaliana kuanza mchakato wa Kusainiwa Hati ya Makubaliano (MoU) kuhusu Ushirikiano kwenye Eneo la Uchumi wa Buluu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news