Balozi Kasike ateta na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Eswatini

MBABANE-Katika kuimarisha uhusiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ufalme wa Eswatini, kwenye Sekta ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Eswatini na Madagascar amekutana na Mhe. Chief Ndlaluhlaza Ndwandwe, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Ufalme wa Eswatini mjini Mbabane.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 28,2024 na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo,Msumbiji.
Wakati wa Mkutano huo, Viongozi hao wawili walikubaliana kuendelea kushirikiana kwenye sekta ya ujenzi wa miundombinu.

Ni kubadilishana utaalamu na uzoefu sambamba na kuangalia uwezekano wa kushirikiana kwenye Sekta ya Usafiri wa Anga hasa baada ya nchi hizi mbili kufanikiwa kufufua mashirika yao ya ndege.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news