CDC Tanzania,Muhimbili zakubaliana

DAR ES SALAAM-Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania, Dkt. Mahesh Swaminathan amesema kituo hicho kipo tayari kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kuambukiza na yasiyoambukiza.
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi.
Dkt. Swaminathan aliyasema hayo jana jioni alipotembelea MNH na kukutana na Uongozi ili kuangalia fursa mbalimbali za ushirikiano kati ya kituo hicho na Hospitali ya Taifa Muhimbili yenye dhamana kubwa katika masuala ya utoaji huduma za kibingwa na ubingwa bobezi, utafiti na elimu kwa ujumla wake kutokana na kuwa hospitali yenye hadhi ya Chuo Kikuu kwenye masuala ya mafunzo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Mohamed Janabi amesema hospitali ipo tayari kushirikiana na CDC Tanzania kutokana na hospitali hiyo kuwa na mifumo madhubuti ya kukusanya taarifa, uwepo wa maabara kubwa yenye vifaa vya kisasa vya kufanya uchunguzi na kufanya tafiti mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news