Dkt.Nchimbi kushiriki maziko ya Askofu Francisca Gachuma

MARA-Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amewasili wilayani Tarime, Mkoa wa Mara, kushiriki maziko ya Askofu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC), Jimbo la Mara Kaskazini, Bi. Francisca Mwita Gachuma, ambaye ni mwenza wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, Ndugu Christopher Mwita Gachuma.
Baada ya kuwasili msibani nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Bomani, Tarime Mjini, leo Ijumaa, Machi 29, 2024, na kupokelewa na Viongozi wa Chama na Serikali, Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi alipata fursa ya kuweka saini kitabu cha maombolezo na kuwapatia pole wafiwa, wakiongozwa na Familia ya Mzee Gachuma, pamoja na kushiriki ratiba ya awali ya msiba, kabla ya mazishi yatakayofanyika Machi 30, 2024, huko Komaswa, Tarime.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news