Dkt.Yonazi:Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kuratibu Programu ya ASDP II kuongeza tija

DODOMA-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameeleza kuwa, Ofisi yake itaendelea kuratibu Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ili kuendelea kuleta tija kwenye sekta hiyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza kuhusu masuala ya ASDP II wakati wa kikao kuhusu Maendeleo ya zoezi la tathmini na uhuishaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo jijini Dodoma tarehe 13 Machi, 2024.

Ameyasema hayo alipokutana na timu ya wataalamu kwa lengo la kujadili Maendeleo ya zoezi la tathmini na uhuishaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) tarehe 13 Machi, 2024 katika ukumbi wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma.

Kikao hicho kilijumuisha wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali, Wasimamizi wa Programu ya ASDP II, Wataalam kutoka AGRA pamoja na Taasisi ya Axum Tanzania.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza kuhusu masuala ya ASDP II wakati wa kikao kuhusu Maendeleo ya zoezi la tathmini na uhuishaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo jijini Dodoma tarehe 13 Machi, 2024.

Dkt. Yonazi ameeleza kuwa adhima ya Serikali ni kuhakikisha Sekta ya Kilimo inaendelea kupewa kipaumbele ili kuinua uchumi wa Taifa na kujiletea maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news