Mama Mariam Mwinyi aendelea kurejesha tabasamu kwa watoto wa kike Zanzibar

ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mhe.Mama Mariam Mwinyi amezindua programu ya kugawa taulo za kike (Tumaini Kits) katika viwanja vya Jadida Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Uzinduzi huo umefanyika Machi 29,2024 huku programu hiyo ikifadhiliwa na Shirika la UNICEF kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu Zanzibar, pamoja na Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) kwa usambazaji wa taulo za kike 1,000 Unguja na Pemba.
Viongozi mbalimbali wameshiriki akiwemo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Lela Mohamed Mussa, Mkuu wa UNICEF Zanzibar Laxmi Bhawani na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news