Spika Dkt.Tulia awajulia hali majeruhi wa ajali mkoani Pwani

PWANI-Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 30 Machi, 2024 amefika katika Hospitali ya Msoga iliyopo Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani kwa ajili ya kuwajulia hali majeruhi.
Ni wa ajali iliyohusisha gari la mashabiki wa Simba na lori la mizigo iliyotokea jana katika eneo la Vigwaza mkoani humo.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia ametoa mchango wa majeneza mawili kwa ajili ya kuwahifadhi marehemu wa ajali hiyo pamoja na kutoa mchango wa shilingi milioni 3 kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi hao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news