Muhimbili yatoa pini kwenye mapafu ya mtoto wa miaka mitano

DAR ES SALAAM-Mtoto mwenye umri wa miaka mitano, mkazi wa jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki ametolewa pini kwenye mapafu yake.
Ni kwa kutumia kifaa maalum chenye kamera kilichopelekwa moja kwa moja hadi ilipo, kuinasa na kisha kuitoa ambayo amekaa nayo kwa takribani mwezi mmoja.

Wazazi wa mtoto huyo (majina yamehifadhiwa) wanasema, mtoto wao alianza kupata kikohozi na homa za mara kwa mara ndipo walipompeleka hospitali kubwa ya binafsi jijini Dar es Salaam ambapo walimfanyia baadhi ya vipimo vilivyoonesha uwepo wa maambukizi kifuan akalazwa.

Kesho yake akafanyiwa kipimo cha X-Ray na kugundua uwepo wa pini ya kubandikia matangazo ambayo walijaribu kuitoa bila mafanikio na kuwashauri wazazi hao kumpeleka ama Kenya au Afrika ya Kusini ili kutolewa pini hiyo.

“Kabla ya kufikia uamzi wa kumpeleka Kenya au Afrika ya Kusini, mme wangu alisema aliona clip kwenye vyombo vya habari kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili hivi karibuni ilifanikiwa kumtoa mtoto Skrubu (Screw)…"

Hivyo waliomba wapewe Rufaa kwenda Muhimbili. "Ambayo tulipewa na kupokelewa vizuri hapo Emergency ya Muhimbili ambao walimfanyia X-Ray na kuona pini ilipokaa na kutuambia kuwa mtoto wanamlaza na atafanyiwa procedure ya endoscope kesho yake,” amesema mama wa mtoto.
Ameeleza kuwa,huduma hiyo ya kumtoa pini ilifanyika vizuri na kwa mafanikio makubwa ambapo mtoto hakohohi tena kama zamani na ni mwenye furaha.

“Huduma zinazotolewa Hospitali ya Taifa Muhimbili ni sawasawa na zile tunazofuata katika hospitali kadhaa, kwani kuna watoa huduma wenye weledi, vifaa tiba vya kisasa, mahali pazuri pa kulala, huduma kwa wateja (customer care) ni nzuri,“amesema mama huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news