Naibu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje ashiriki Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu SADC

LUANDA-Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 4 hadi 5 Machi, 2024.
Kikao hicho kitafuatiwa na kikao cha Kamati ya Fedha tarehe 6 Machi, 2024 ambapo kwa pamoja vikao hivyo ni maandalizi ya Baraza la Mawaziri litakalofanyika tarehe 10 - 11 Machi, 2024 jijini Luanda, Angola.
Aidha, pamoja na masuala mengine, vikao hivyo vya awali vitapokea na kujadili taarifa mbalimbali ikiwemo Tathmini ya utekelezaji wa maamuzi ya Mikutano iliyopita, Hatua iliyofikiwa katika kugharamia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maendeleo wa SADC wa 2020–2030, Taarifa ya Kamati ya Fedha, Taarifa ya Kamati ya Rasilimali Watu na Utawala na Hatua iliyofikiwa katika kutafsiri nyaraka muhimu za SADC kwa lugha ya Kiswahili.
Kauli mbiu ya Baraza la Mawaziri la mwaka huu ni ‘’Rasilimali Watu na Fedha: Nyenzo muhimu kwa ukuaji Endelevu wa Viwanda katika Kanda ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news