Askari wa Kikosi cha Mbwa na Farasi wapeleka tabasamu kwa wagonjwa Hospitali ya Zakhiem

NA ABEL PAUL
Tanpol

ASKARI Polisi wa kike Kikosi cha Mbwa na farasi makao makuu Dar es salaam wameendelea kuyakumbuka makundi ya wahitaji licha ya kuwa na dhamana ya kuwalinda raia na mali zao ambapo wamewafariji wagonjwa katika Hospitali ya Zakhiem iliyopo Mbagala Wilaya Temeke Mkoa wa Dar es salaam na kutoa vitu mbalimbali.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Khadija Maulid ambaye aliwaongoza askari wa kike kwenda hospitali ya zakhem kutoa misaada ya vitu mbalimbali ambavyo waliona vitakuwa msaada kwa wahitaji hao ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

Ameongeza kuwa, kuelekea Siku ya Wanawake Duniani wameona ni vyema wao kama kundi la askari wa kike wa kikosi cha Mbwa na farasi kuliangalia kundi hilo la wahitaji na kutoa kile walichobarikiwa kutoa kwa wahitaji hao.
Mkaguzi huyo amebainisha kuwa wamekuwa na utaratibu huo mara kwa mara kama kikosi Cha Mbwa na farasi Makao Makuu ambapo wamekuwa wakitembelea makundi mbalimbali ya wahitaji katika jamii.

Pia,Mkaguzi Khadija ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kufika Makao Makuu ya kikosi cha Mbwa na farasi kujifunza mambo mbalimbali kuhusiana na wanyama Mbwa ambao wamekuwa wakiwatumia katika ulinzi wa makazi yao.
Sambamba na hilo amewakumbusha kuwa wanyama hao ambao hutumika katika ulinzi ni vyema wakawatumia wataalamu wa Jeshi la Polisi kuwafundisha ili wawe walinzi wazuri huku akiwakumbusha swala la chanjo kwa wanyama hao kuwa ni muhimu ili kuepusha magonjwa ya kichaa cha Mbwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news