Rais Dk.Mwinyi ateta na Nadal Al-Nashif

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Nadal Al-Nashif na ujumbe wake Ikulu Zanzibar.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amekutana Naibu Kamishna huyo Machi 9,2024 Ikulu jijini Zanzibar.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema, Zanzibar imemairisha ushirikiano katika kuzijengea uwezo taasisi za kisheria hususani utekelezaji wa sheria, Mahakama na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka.

Naye Naibu Kamishna Nadal Al-Nashif amesema, wataisaidia Zanzibar katika kuwajengea uwezo hususani taasisi za kisheria.

Vilevile katika mazungumzo yao wamezungumzia nafasi ya Vyombo vya habari, huduma za maendeleo ya kijamii, utalii, Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na uwezeshaji wa wanawake na vijana .

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news