Tanzania ina sheria nzuri-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania imeweka sheria nyingi zinazozuia urasimu katika kupata huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za kisheria.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Machi 8,2024 wakati akifunga Mkutano wa siku tano wa Mawaziri wa Sheria kutoka katika Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola uliofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip,Uwanja wa ndege Zanzibar.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi amewakaribisha Tanzania wawekezaji kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kuchangamkia fursa za uwekezaji hususan katika uchumi wa bluu, sekta ya utalii, uwekezaji wa miundombinu, madini, kilimo, na sekta ya afya.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amesema sheria hizo zinawawezesha wananchi kupata huduma bila ya kuwepo na urasimu lakini pia zinatoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza katika nyanja mbalimbali bila usumbufu.

Rais Dkt. Mwinyi amesema, Mifumo ya Kidigitali italeta mabadiliko makubwa katika sekta ya Sheria ambapo haki kutolewa kwa haraka kwa kuwa mashahidi hawatalazimika kufika mahakamani kutoa ushahidi, watatoa ushahidi walipo, Jaji atatoa hukumu popote alipo pia.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameitaka Jumuiya ya Madola kuendelea kusimamia sheria na kuhimiza nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kuwa na sheria rafiki zinazoendana na ulimwengu wa kidijiti kwa kutoa fursa kila mtu kutambua haki zake.

Vilevile wajumbe wa Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali wamepata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii Zanzibar pia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland KC amehudhuria mkutano huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news