Serikali yazindua afua kabambe ya Mfumo Jumuishi wa Kupambana na Unyanyapaa

DAR ES SALAAM-Serikali imesema licha ya jitihada mbalimbali kutekelezwa katika kukabiliana na UKIMWI, suala la unyanyapaa, limeendelea kuwa sababu kuu ya kutoyafikia malengo hayo.
Mganga Mkuu wa Serikali ameyasema hayo kwenye taarifa yake iliyosomwa na Mkuu wa Programu kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Catherine Joachim, katika uzinduzi mradi wa afua ya mfumo jumuishi kwa watoa huduma za afya kupunguza unyanyapaa kwa Watu wanaoishi na Virusi vya Ukiwmi (WAVUI).

“Kupunguza unyanyapaa na ubaguzi katika vituo vya kutolea huduma za afya, kunaweza kuchangia kufikia lengo hilo, kwa kuwafikia WAVIU na ambao wapo kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo.

“Mradi wa afua ya mfumo jumuishi hapa Muhimbili ikiwa ni fursa ya kuwaleta pamoja wadau mbalimbali nchini pamoja na kuongeza uelewa, kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU),” alisema Dkt. Catherine akisoma taarifa hiyo jijini Dar es Salaam.

Alisema, mradi huo utagharimu shilingi bilioni 2,347 na kwamba kwa mujibu wa Malengo Endelevu ya Dunia (SDGs-2030), miaka sita ijayo inategemewa kudhibiti na kutokomeza UKIMWI.

“Ripoti ya kimataifa iitwayo ‘Njia ya Kumaliza UKIMWI’ inaonyesha kuwa kumaliza UKIMWI ni uamuzi wa kisiasa, kifedha na nchi pamoja na viongozi wanaofuata njia hizo tayari wameshaona matokeo makubwa.
“Inasema nchi ambazo tayari zimeanza kushuhudia mafanikio hayo ni Botswana, Eswatini, Rwanda, Tanzania na Zimbabwe ambazo tayari zimefikia malengo ya ‘95-95-95’,” alisema.

Alisema,mfumo huo unafafanua, asilimia 95 ya kwanza ni kwa watu wanaoishi na VVU wajue hali zao za maambukizi, asilimia 95 nyingine ya watu wanaoishi na VVU wapate matibabu na asilimia 95 ya watu waliokuwa kwenye matibabu wawe wamefubaza VVU.

Mradi huo unaofadhiliwa na Bill & Melinda Gates, utahusisha uboreshwaji wa mitaala sita pamoja na mafunzo kwa watoa huduma za afya takribani asilimia 70 kutoka katika hospitali nufaika za mradi unatekelezwa Zambia, Ghana na Tanzania kwa miaka mitatu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, tangu alisema tangu kugundulika kwa ugonjwa huo, suala la unyanyapaa na ubaguzi limeendelea kuwa kikwazo katika jitihada za kidunia.

“Madhumuni ya kutekeleza afua hii ni kupunguza unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya WAVIU kwenye vituo vya afya. Hii itawawezesha kuzifikia huduma endelevu hivyo kuboresha matokeo chanya ya huduma za VVU na UKIMWI,” alisema Prof. Janabi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news