Waziri Keul azindua kitabu cha maisha ya tamaduni za Kichaga kilichoandikwa kwa Kiswahili



KILIMANJARO-Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul ameshiriki uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la Kichaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kisare Makori (kulia) na Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt. Resani Mnata wakizindua kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili katika hafla iliyofanyika Old Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 01 Machi 2024.
Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt. Resani Mnata akimkabidhi nakala ya kitabu mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi.Naomi Zegezege katika hafla ya kuzindua kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

Wakati wa uzinduzi ambao umefanyika katika kigango cha Kidia, Old Moshi, imeelezwa kuwa kitabu hicho ambacho kimetafsiri kazi ya mwandishi mchungaji Bruno Gutmann, kinalenga kutambua utumishi wa mchungaji huyo raia wa Ujerumani ambaye aliishi eneo hilo kwa miaka 28 na kushirikiana na wananchi wa maeneo hayo huku akieneza injili.

Kitabu hicho ni miongoni mwa vitabu 400 vilivyoandikwa kwa lugha ya Kijerumani na mchungaji huyo ambapo mpaka sasa vitabu vitano vimeandikwa kwa lugha nyingine ikiwemo kichaga na kiswahili.
Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni na washiriki wa hafla ya uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akiweka shada la maua katika kaburi la Mangi Meli aliyeuawa na wakoloni wa kijerumani wakati wa utawala wao.
Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kisare Makori (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo Dkt. Resani Mnata , Balozi wa Tanzania Ujerumani (wa pili kulia) wakitoa heshima katika kaburi la Mangi Meli aliyeuawa na wakoloni wa kijerumani wakati wa utawala wao.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta (wa pili kulia) aliposhiriki hafla ya uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili iliyofanyika Old Moshi mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

Uzinduzi huo pia umeshuhudiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kısare Makori, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Hassan Mwamweta na Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Resani Mnata.

Naibu Waziri Keul yuko nchini kwa ziara ya siku nne ya kikazi kuanzia tarehe 29 Februari hadi Machi 4,2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news