BUJUMBURA-Mawaziri wa Sekta ya Madini wa Burundi, Mheshimiwa Mhandisi Ibrahim Uwizeye na Tanzania Mheshimiwa Anthony Mavunde leo wamesaini hati ya makubaliano ya kushirikiana kwenye sekta ya madini ili kukuza mchango wa sekta hii katika uchumi wa nchi mbili hizi.
Hafla ya kusaini makubaliano hayo imefanyika leo jijini Bujumbura,Burundi na kuhudhuriwa na watalaamu wa nchi zote mbili.
Maeneo ya Ushirikiano yanajumuisha;
- Ujenzi wa Viwanda vya Uchenjuaji na Usafishaji wa Madini.
- Kubadilishana Uzoefu na utaalamu katika utafiti wa kina wa madini.
- Kuongeza thamani ya madini kwa kuzalisha bidhaa zitokanazo na madini.
- Kujenga uwezo wa kitaasisi na wataalamu wa pande zote mbili.
- Kusimamia sheria na taratibu za biashara ya madini inayohusisha pande zote mbili.
Akitoa maelezo ya awali Waziri wa Maji,Nishati na Madini wa Jamhuri ya Burundi,Mheshimiwa Mhandisi Ibrahim Uwizeye amesema nchi ya Burundi na Tanzania zimekuwa na urafiki wa muda mrefu na mahusiano mazuri.
Hivyo,ni muhimu kutumia fursa hii kushirikiana kwenye sekta ya madini ili sekta hii itoe mchango unaostahili katika kukuza maendeleo ya uchumi wa Burundi na Tanzania chini ya uongozi imara wa marais Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye (Burundi) na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan (Tanzania).

Pia, kutumia huduma ya Kiwanda cha Usafishaji madini ambacho kitajengwa katika eneo la ulipokuwa Mgodi wa Buzwagi wilayani Kahama mkoani Shinyanga.