VIDEO:DC wa Mkuranga atuhumiwa kuwafanyia ubabe viongozi, chama tawala ampiga 'stop' Mbunge kutoa misaada

PWANI-Hali ya sintofahamu imetokea Mkoa wa Pwani,Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga baada Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Pwani,Hawa Mchafu Chakoma kupokea zuio kutoka kwa Mkuu wa wilaya hiyo, Khadija Nassir Ali la kutopokelewa vifaa vya afya alivyokuwa amepeleka katika Kituo cha Afya cha Msorwa.
Ikiwa ni katika juhudi za kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan za kusaidia kuimarisha Sekta ya Afya.

Hata hivyo, Diwani wa Kata ya Mbezi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Rashid Selungwi kwa niaba ya madiwani wenzake alionesha msimamo wake wa kupokea vifaa hivyo kwa niaba ya madiwani wenzake na kusema kuwa vifaa hivyo watavipeleka katika ngazi za juu za CCM kuwaeleza kadhia hiyo iliyowakumba.
Aidha, Selungwi amesema imekuwa muendelezo wa mkuu huyo wa wilaya kuingilia majukumu ya watendaji kwa kuwakataza mambo mengi.Taarifa kamili tembelea YouTube channel ya ManaraTv.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news