DAWASA:Kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji Machi 5 hadi 7

DAR ES SALAAM-Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imewatangazia wateja na wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini kuwa, kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji kwa baadhi ya maeneo ili kuruhusu maboresho ya msingi katika mtambo.
Siku ya Jumanne Machi 5,2024 kuanzia saa 12 jioni hadi siku ya Alhamisi Machi 7,2024.

Maeneo yatakayoathirika na upungufu huu wa huduma ya maji ni;

Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Kunduchi, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Madale, Goba, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu UDSM, Mwenge, Chuo Kikuu Ardhi, Kijitonyama, Mikocheni,

Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya Jiji.

DAWASA inawashauri wananchi kuhifadhi maji ya kutosha katika kipindi cha matengenezo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news