Watumishi wanawake mna mchango mkubwa TARURA-Mbilinyi

DODOMA-Imeelezwa kwamba watumishi wanawake wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) nchini wana mchango mkubwa katika kufanikisha utekelezaji wa majukuu ya taasisi hiyo.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa TARURA Bi. Azmina Mbilinyi wakati wa sherehe za pamoja kwa watumishi wanawake ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika ukumbi wa Royal Village jijini Dodoma

“Nawapongeza wanawake wote na kuwatia moyo kwamba tunatambua mchango wenu mkubwa mnaofanya katika kuhakikisha utekelezaji wa kazi za taasisi unafanikiwa."
Amesema, anatamani wanawake hao siku moja wawe viongozi wakubwa na wengine kuwa ni mameneja TARURA ama sehemu nyingine katika utumishi wao.

“Chapeni kazi kwa msaada wa Mungu mnaweza kufanya mambo makubwa wote mnaweza."

Kwa upande mwingine Mkurugenzi huyo aliwaasa wanawake hao kutumia muda wao katika kuangalia familia licha ya muda mwingi kuwepo kazini.
“Hivi sasa yapo matatizo makubwa sehemu tunazoishi ikiwemo unyanyanyasi wa watoto, kwa hiyo pamoja na majukumu mengi mliyonayo kazini mnapaswa pia muangalie familia zenu katika makuzi na malezi kwa watoto wetu ili waje kuwa baba na mama bora hapo baadae,”alisisitiza Bi. Azmina.

Hata hivyo aliwashauri wanawake hao kuwekeza baadhi ya mifuko ya uwekezaji pamoja na kuthubutu kwa kuanzisha biashara ambazo zitawaongezea vipato vya ziada.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na watumishi wanawake kutoka TARURA Makao Makuu pamoja na ofisi za mameneja wa Mikoa na Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news