Rais Dkt.Samia afanya mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa,wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi ambapo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amehamishwa kutoka mkoa huo na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Mpogole Kusiluka ambapo imeeleza kuwa, Rais Dkt. Samia pia amemhamisha Halima Omar Dendego kutoka Mkoa wa Iringa kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Aidha, Peter Joseph Serukamba amehamishwa kutoka Mkoa wa Singida kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Wakati huo huo, Balozi Batilda Salha Burian amehamishwa kutoka Mkoa wa Tabora kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Vile vile Rais Dkt.Samia amemteua Daniel Chongolo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Chongolo aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo miezi kadhaa iliyopita alijiuzulu nafasi hiyo.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa Rais Dkt.Samia amemteua Patric Kenan Sawala kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Sawala alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba.

Naye Paul Matiko Chacha ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi;






Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news