CPA Makalla amrithi Makonda,Mongella ndiye Naibu Katibu Mkuu,Ally Hapi apelekwa Wazazi na Jokate arudishwa UVCCM

DAR ES SALAAM-Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo Aprili 3, 2024 Jijini Dar es salaam, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na masuala mengine imemchagua ndugu John Mongella kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichokutana leo Jumatano, Aprili 2024, jijini Dar Es Salaam.

Ndugu Mongella anachukua nafasi ya Anamringi Macha ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Pia, imemchagua Amos Gabriel Makalla kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, akichukua nafasi ya ndugu Paul Makonda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Vile vile,Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imemchagua Jokate Urban Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, akichukua nafasi ya Fakii Raphael Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Wakati huo huo Ally Hapi, ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania, akichukua nafasi ya Gilbert Kalima ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news